Sukuma – NTALE OSI NYERERE NA NZALA

 

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu     Edited by: Fr. Zakaria Kashinje OSA

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Ng´waka 1974 Itanzania igabhiza ni yanga lwa nzala. Bhanasi bhagayisaila iSelekari kulwa nguno ya kugaiwa ginhiwa jiliwa. Iki jiliwa ja nzala jalijahujumiwa na bhanhu abho bhagimana bhoi duhu.

Ku iniyo, abhanasi bhagapandika iyange itale. Jililo ja abho abhatina nguvu, jiganshigila úntale o si, ung´walimu Julius Nyerere.

Aho owigwa ubhulalamiki bhobho, wamua gugayelela ama mabhelele gose ayo gatumikaka umugujitula ijiliwa ja gubhagabhila bhule ung´wishirika lya si lwa bhushisha (NMC).

Lushiku lumo aho ali kunjini go Shinyanga, Ung´walimu agita jito ja gubhashesha abhanhu, ja guzwala majitambalala makulukulu na ngofila ubhi giti munhu ung´wilombeleja.

Aho oshika aha nyango go NMC, nduhu munhu nulu umo uyo agamhana. Wishebeleja lumo na lumo mpaga mu ofisi ya ng´wa meneja, bho nduhu guzunulijiwa tamu.

Agapiga hodi aha nyango na guhamuka aliyomba, “Aying´we bhanhu umugati umo!” “Nambilijagi, natina jiliwa ukukaya yane!” Meneja unshokeja, “Lekaga gudukoya namhala ebhe! Ingaga ahenaha! Jaga jako uko isoko ugigulile ijiliwa. Kihamo ni iniyo, Nyerere agendelea gubhikumbilija, “Bhabehi, nambilijaji! Nagucha na nzala.”

Aliyo bhadandegelekile, umeneja na bhambilija bhakwe, bhagendelea kujinja mubei ya higulwa na bhasuluja abha bhagashika ho gugula ijiliwa jenijo ja nzala, ijo jalijidakililwa kugabhanyiwa bhule ku bhanasi abho bhalibhadinajo.

Gashinaga ili nghana igiki,Uo lwiguto adanmanile uo nzala.

Inghalikilo yaho, Unyerere agagufungula unyango na gwingila muofisi. Wangu wangu agakungula amajitambalala na ngofila yenuyo, na heneho, wimanyicha kubhoi igiki ali nani, bho nduhu guyomba mhayo gosegose. Pye bhuding´wa na bhujinjimazu, bho gukumya!

Aho Ntale osi Nyerere oshoka Dar es salama, igatangajiwa giki, umeneja ng´wenuyo na bhambilija bhakwe, bhapejiwagwa imilimo ya gubhatumamila abhanhu kulwa nguno ya juhuma iyo bhagiyita.

Tukio La Rais Nyerere Na Njaa.
Mwaka 1974 Tanzania iliandamwa na janga la njaa. Wananchi waliilalamikia serikali kwa vile walikosa kupewa chakula. Kwani kile chakula cha njaa kilihujumiwa kwa maslahi ya watu binafsi.

Hivyo, wananchi walipata usumbufu mkubwa. Kilio cha wanyonge kilimfikia Rais Mwalimu Julius Nyerere. Baada ya kuyasikia malalamiko yao, akaamua kuyatembelea maghala yote yaliyotumika kuhifadhia chakula cha kugawa bure kwenye shirika la Taifa la Usagishaji (NMC).

Siku moja akiwa mjini Shinyanga, Mwalimu Nyerere alifanya vioja kwa kuvaa matambara na kofia kuukuu kama omba omba. Alipowasili kwenye lango la NMC, hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kumtambua. Akajipenyeza moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya meneja, bila ya kupata kibali kwanza.

Alipiga hodi mlangoni na kupaza sauti akisema, “Enyi watu ndani humo!” Nisaidieni, sina chembe ya chakula nyumbani kwangu!” meneja akamjibu, “Acha kutubughudhi mzee wewe! Ondoka hapa! Nenda zako huko sokoni ukajinunulie chakula. Hata hivyo, Nyerere aliendelea kuwasihi, “Jamani, nisaidieni! Nitakufa kwa njaa.

Lakini kwamwe hawakumsikiliza, badala yake, meneja na wasaidizi wake wakaendelea kulangua na wafanyabiashara waliofika kununua kile chakula cha njaa ambacho kingepaswa kugawiwa bure kwa wananchi wahitaji.

Kumbe ni kweli kwamba:
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

Mwishoni, Nyerere aliufungua mlango na kuingia ofisini. Ghafla akavua yale matambara na ile kofia, na hapo hapo akajidhihirisha kwao kuwa ni nani, bila ya kusema neno lolote. Wote walishikwa na butwaa!

Baada ya Rais Nyenye kurejea Dar es Salaam, ilitangazwa kwamba yule meneja na wasaidizi wake waliwajibishwa kwa kufukuzwa kazi kwa hujuma.

This entry was posted in Sukuma and tagged , , , . Bookmark the permalink.

Comments are closed.